NYIMBO ZA MAKABILA YETU 1 - WASUKUMA (MAREHEMU NG'WANAKANUNDO - MWANZA)

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Thursday, March 10, 2011

RAIS KIKWETE ALIPOONJA UTAMU WA NGOMA ZA KISUKUMA

  • Wamasai na Watindiga ni mojawapo ya makabila yanayovuma sana kwa kuendelea kudumisha utamaduni wao - japo nayo yananyemelewanyemelewa na utandawazi. Wasukuma nao bado wanajikongoja na mojawapo ya mambo wanayoendelea kuyadumisha ni utamaduni wao wa kucheza ngoma zao za kienyeji.
  • Kule wilayani Bariadi, kwa mfano, kila tarehe 30 mwezi wa tano makundi makuu mawili kinzani ya Bagika na Bagalu hukutana na kushindana usiku mzima na mshindi huamuliwa nyakati za mchana majira ya saa 11 siku inayofuatia. Mashindano haya huvutia watu wengi sana na yamekuwa kama sehemu ya sikukuu kwa Wanyantuzu. Katika mashindano haya mamanju huonyesha ubingwa wao wa madawa na uchawi; na anayeelemewa ndiye hushindwa.
  • Kama mkereketwa wa maswala ya utamaduni, nimefurahi kumwona Mh. J.K. akifurahia ngoma hizi za Kisukuma siku alipotembelea makumbusho ya Wasukuma yaliyoko Bujora jijini Mwanza.  
  • Utamaduni ndiyo utambulisho wetu hapa duniani na mtu asiye na utamaduni wake mwenyewe ni mtu aliyepotea na asiyejielewa. Japo utamaduni wetu umo katika pigano na unatishwa kuangamizwa na utandawazi, inafurahisha sana kuona kwamba baadhi ya vipengele vyake kama hiki cha michezo ya jadi vinazidi kudumishwa. Tusonge mbele.
J.K. akiangalia majina ya Watemi. Picha zote kutoka Blogu ya Ikulu.

*****...******

Msikilize Ng'wanakanundo hapa chini, manju mashuhuri wa Kisukuma kutoka Mwanza.

Monday, February 21, 2011

WIMBO MFUPI WA KISUKUMA

....Shiliwa shiswe shazugagwa siza, shokejagi msiginogelwa...
...chakula chetu kimepikwa vizuri, msichoke kurudia tena...